Ilani ya Kisheria na Masharti ya Matumizi (Disclaimer & Terms of Service)
Ilani ya Kisheria na Masharti ya Matumizi (Disclaimer & Terms of Service)
Jukwaa hili linaendeshwa kama kitovu cha kidijitali cha kuunganisha watafutaji nyumba, wamiliki, na mawakala mkoani Moshi. Kwa kutumia blogu hii, unakubaliana na masharti yafuatayo:
1. Uhakiki wa Taarifa (Limitation of Liability)
Ingawa timu yetu inafanya mchakato mkali wa kuhakiki kila tangazo (Verified Badges), watumiaji (wapangaji) wanashauriwa kufanya ukaguzi wa kina wa nyumba physically kabla ya kufanya maamuzi yoyote ya kifedha. Jukwaa hili halitawajibika kwa hasara, utapeli, au migogoro yoyote ya kisheria itakayotokea nje ya mfumo wetu.
2. Usalama wa Malipo (Payment Safety Warning) Tahadhari:
Ni marufuku kutuma pesa ya amana (Deposit) au kodi ya nyumba kwa njia ya simu (M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money) kwa mtu yeyote kabla ya Kufika kwenye eneo la nyumba na kuikagua wewe mwenyewe. Kuthibitisha umiliki halali wa mtu unayemlipa.
Kusaini mkataba halali wa upangaji mbele ya mashahidi wa kisheria au viongozi wa mtaa.
3. Haki ya Kuondoa Matangazo (Right to Terminate)
Tuna haki ya kufuta tangazo lolote, kuzuia namba ya simu, au kumfungia mtumiaji (dalali au mmiliki) mara moja bila taarifa yoyote iwapo itagundulika kuwa ametoa taarifa za uongo, amekiuka maadili ya kazi, au ameripotiwa na wateja kwa tabia za utapeli au lugha chafu.
0 Comments:
Post a Comment